Thursday, September 29, 2011

MAONYESHO YA NNE YA SWAHILI FASHION WEEK YAZINDULIWA RASMI


SWAHILI FASHION WEEK SASA YAWA MAONYESHO MAKUBWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
SWAHILI FASHION WEEK KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA
Swahili Fashion Week ambayo ni maonyesho makubwa Afrika Mashariki na Kati, yakiwa  mwaka kwenye wake wa nne yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa  tarehe 10, 11 na 12 mwezi wa Novemba 2011 Dar es Salaam, Tanzania .
Swahili Fashion Week 2011 itawaleta pamoja wabunifu 50 wa mavazi na vishaufu kutoka nchi ziongeazo Kiswahili na nchi nyingine mbali mbali kuonesha ubunifu wao wa hali ya juu na kuonesha mitindo mipya ya mavazi.
“Kwa mwaka huu tumekua maradufu kwani tuna jumla ya wabunifu 21 waliobobea kutoka Tanzania, wabunifu 10 wanaochipukia kutoka Tanzania, na waliosalia wanatoka katika nchi mbali mbali duniani na kwa ujumla wao wanakua wabunifu 50, ambao watakao jiunga na watanzania wote kusherehekea miaka 50 ya UHURU wa nchi yetu.” Alisema Mustafa Hassanali, Mwanzilishi wa maonyesho ya Swahili Fashion Week.
Pamoja na kuwa na maonyesho ya ubunifu wa mavazi kutakua na Maonyesho ya Manunuzi ya bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa Tanzania yalioyoanzishwa mwaka 2010, kwa mara nyingine maonyesho haya yatakua kivutio kikuu katika Swahili Fashion Week. Mpaka hivi sasa, maonyesho haya yana washiriki 30 waliojisajili kushiriki, nahii inafanya maonyesho haya kua maonyesho makubwa nchini.
Kama tulivyokua wa kwanza kuanzisha Maonyesho ya mavazi kama haya, kwa mara nyingine tena tanakua wa kwanza kuanzisha tuzo katika sekta hii ya ubunifu Afrika ya Mashariki na Kati. Kusheherekea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hii ya ubunifu wa mavazi. Kutakua na Mashindano ya Ubunifu wa Fulana ambayo pia ni ya kwanza, kama njia ya kuwashirikisha vijana na vipaji vyao kama njia ya kukuza sekta hii ya familia hii ya wabunifu.
Pia kuna matukio mbali mbali yanayoandaliwa na na yatafanyika kulekea  kwenye maonyesho haya ya Swahili Fashion Week. Kwa kuanza kutakua na maonyesho ya mavazi jijini Arusha ambayo ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 8 mwezi Oktoba 2011 kama njia moja wapo ya kupelekea na kusambaza kazi za ubunifu katika mikoa mingine ya Tanzania .
Swahili Fashion week 2011, itakua inarushwa hewani moja kwa moja kupitia tovuti ya http://www.swahilifashionweek.com/ kuwapatia fursa wanahabari wa ubunifu duniani kote na kuwajulisha yanayojiri katika ulimwengu wa ubunifu Afrika Mashariki. Maonyesho haya ya moja kwa moja kutoka Makumbusho ya Taifa yatawapatia fursa Watanzania waishio ughaibuni nafasi ya kuunganika na Watanzania wote katika kusheherekea miaka 50 ya UHURU. 
“Tukiwa na malengo ya kukuza biashara hii ya ubunifu katika ukanda huu, ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washirika wetu wote, waliotudhamini katika miaka iliyopita mpaka wakati huu, na pia tungependa kuchukua fursa hii kuhamasisha makampuni na mashirika mbali mbali kujitokeza na kutuunga mkono kwa kudhamini maonyesho haya ya Swahili Fashion Week” Alimalizia Mustafa.
Swahili Fashion week 2011 imedhaminiwa na Nyumba ya Swahili Fashion Week – Hoteli ya Southern Sun, EATV & East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza la Sanaa Taifa), Amarula , Ultimate Security, REDDS Original, Image Masters, Global Outdoor ltd, Vayle Springs ltd, Eventslites, Nipashe, Perfect Machinery ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degree.

HAPPY BIRTHDAY MY LOVE

Darln on ur special day, I wish you all that you desire, May god bless you with love and care. Enjoy every moment, every day of your life. 
Happy Birthday bby.... Much love cwteeee

Wednesday, September 28, 2011

NEWS DESIGNER IN TOWN

 Ni mwanamitindo mdogo anayechipukia, anasoma shule ya secondary Andrew Faza hapa akionyesha mavazi aliyoyadizain katika Baraza show




Thursday, September 15, 2011

MHE.SOPHIA SIMBA AZINDUA RASMI TWENDE

 Muanzilishi na muandaaji wa TWENDE Mustafa Hassanali akiongozana na Waziri wa maendeleo, jinsia na watoto Mhe. Sophia Simba kuelekea kwenye ufunguzi rasmi wa TWENDE.
 Mhe. Sophia Simba akihutubia kuhusiana na wanawake kwenye uzinduzi wa TWENDE.
 Mhe.Simba akitembela kati ya moja ya mabanda ya wajasiriamali wanawake katika ufunguzi wa TWENDE.
 Mmoja kati ya wajasiriamali kina mama akimpa maelezo Waziri Wa maendeleo,jinsia na watoto,Mhe. Sophia Simba,kuhusiana na bidhaa yake katika ufunguzi wa TWENDE
Baadhi ya wajasiriamali wakimulezea mmoja wa wahudhuriaji kuhusiana na bidhaa zao katika ufunguzi wa TWENDE

Wednesday, September 14, 2011

XUL NDO KILA KITU MAMIII

All th best my aunt Halima.....Inshaallah mungu akujalie ufiki hadi mavyuo vikuuu usisahau mwanzo mgumu....love u

MWILI HAUJENGWI NA TOFALI

 Ful kujipendelea....kitu cha chips thamaki na naniiiii baridiiiiii
mmmmh kweli mwili haujengwi na tofali jamanii

Saturday, September 10, 2011

SARHA ISRAEL NDIO VODACOM MISS TANZANIA 2011

 Vodacom Miss Tanzania 2011 Sarha Israel baada ya kutangazwa mshindi akiwa pamoja na mshindi wa pili Tracy Sospeter(kulia) na mshindi wa 3 Alexia William.
Vodacom Miss Tz 2010 aliyemaliza muda wake Genevive Mpangala akimvisha taji Vodacom Miss TZ 2011 Sarha Israel baada ya kutangazwa mshindi.

NANI KUNYAKUA TAJI LA VODA MISS TZ 2011?

Warembo wanaoshiriki Vodacom Miss Tanzania 2011 katika picha ya pamoja. Shindano ili linafanyika leo usiku katika ukumbi wa Mlimani City... swali kwa Watanzania wengi ni NANI KUWA MSHINDI USIKU HUU???

AFRICAN DRESS

KIKI'S DESIGNS


...big up Kiki

AFRICAN SUIT 4MEN

 So nice....i will desgn 4u boyfriend
nice jeaz....lol i love it.

ITS ALL ABT FASH.....

Mmmmmh
nuthng to say

SLIM GAL

 Shes slim gal dic iz kind of modelz i wat, do u thnk ur lookng like this please contact with me....mkehela72@yahoo.com

Monday, September 5, 2011

SELECTION YA NEW MODELZ IN ROLLING AT KINO

 
Mwanamitindo Mariam Mogella yupo kwenye selection ya models kwa sasa kama ww ni msichana mwenye umri kuanzia miaka 16 hadi 25 na una malengo ya kuwa model wasiliana na Princess Mamu Best kwa mail....mkehela72@yahoo.com
 

Sunday, September 4, 2011